Monday, October 25, 2010

Sensei NANTAMBU KAMARA BOMANI

    Sensei Bomani alianza mafunzo yake ya karate miaka ya 60.Mpaka mwaka 1968 Bomani alikuwa ameshakwenda Okinawa Japan kujifunza na kufundishwa na Seinsei Eichii Myazato,Sensei Bomani alikuwa mwanafunzi wa Sensei Eichii Miyazato mpaka miyazato alipofariki mwaka 1999.

Miaka ya mwanzoni ya 1970 Sensei Bomani alifungua dojo yake ya mwanzo Ithica,New York.Bomani pia ndio aliyeleta Jundokan tanzania na Africa kwa ujumla.Alianzisha na kufungua shule ya kwanza ya gojuryu jundokan dar es salaama mwaka 1973 na kuanziasha Tanzania Okinawa Gojuryu Karate association.Sensei Bomani pia alikuwa MUHIMILI mkubwa wa kueneza jundo kan gojuryu marekani.Alianzisha dojo nyingi katika majiji ya New York,Washington,Kentucky na Ohio.Ameacha wanafunzi waandamizi YUDANSHA/SENPAIS,mimi nikiwa mmojawapo katika africa na marekani.Alianzisha pia Okinawa Gojuryu Karate-do Kyokai Jundokan USA na kutumika kama rais wa kwanza wa chama hicho pia alianzisha West Africa Okinawa Gojuryu Karate-do Kyokai.Dojo zake nyingi bado ziko na zinaendelea kusambaza filosofia ya traditonal okinawa gojuryu.

Sensei Bomani aliendelea kushirikiana na Dojo zake nyingi alizozianzisha africa na marekani pia kusafiri kwenda okinawa kwa mafunzo zaidi.Madaraja yote ya vyeo vyake katika rank za gojuryu dan nane 8th dan
 alipewa na sensei Eichii Miyazato,Kati ya wanafunzi wake wakuu waandamizi wa tanzania ni,Daudi Magoma,Mabruki,Geoffrey Shoo,Brighton Manyau,Pascal Irungu,Heri Kivuli,Marehemu Bofu kwambwa,Geoffrey Mbezi,Alfred Malekia na wengine weeeeeeengi amabo mpaka leo kwa namna moja au nyingine wanaendelea kuisamba za Gojuryu Tanzania.

Mwezi August 2009 Seinsei Bomani alifariki kwa ugonjwa wa moyo,alizikwa katika jiji la Accra Ghana Africa ya magharibi.Sensei Bomani alikuwa muhimili mkubwa na muasisi wa Gojuryu africa na Marekani NA aliktunukiwa dani ya 9 9th dan,kwa juhudi zake binafsi na mapenzi ya gojuryu alisambaza karate katilka mabara haya mawili ya Africa na Maekani.Kwangu alikuwa mwalimu Mkuu,Rafiki,Role model and ispiration,.BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

No comments:

Post a Comment